Karibu!

Karibu rafiki! Ninaitwa Mackenzie. Mimi ni mwanafunzi Washington University mjini St. Louis katika jimbo la Missouri. Ninafanya blogu hii kama maradi wa mwisho wa darasa langu la kiswahili. Ninatumaini unapenda maagizo ya upishi yangu! Asante sana kwa kusoma blogu yangu. Nina blogu ya kupika nyingine katika kiingereza, uangalie: http://neverskipdessertbymackenzie.wordpress.com

Tuesday, December 10, 2013

Maagizo ya Upishi wa Mkate wa Viazi Vitamu

Mwaka uliopita, nilipika viazi vitamu kila wakati. Nilivipika katika kila kitu! Siku moja, nilifikira kuweka viazi vitamu katika mkate. Nilipenda ndizi katika mkate wa ndizi kwa hivyo, pengine viazi vitamu katika mkate vitakuwa vizuri pia! Niliupopika mkate ulikuwa mzuri sana na mimi na rafiki yangu tuliupenda! Sasa, ninapika mkate huu kila wakati. Pia, mwaka uliopita niliupika kutoka darasa la kiswahli na wanafunzi waliupenda! 


Viungo:
  •  kikombe kimoja na nusu cha unga
  •  kijiko cha chai kimoja cha chumvi
  •  kijiko cha chai kimoja cha soda ya kuoka
  •  kijiko cha chai kimoja nusu cha hamira
  •  kijiko cha chai kimoja nusu cha mdalasini
  •  kijiko cha chai kimoja nusu cha kungumanga
  •  ndani ya kiazi kitamu kimoja
  •  kikombe thelathi mbili cha sukari
  •  kikombe theluthi moja cha sukari ya kahawia
  •  vijiko vya mezani sita vya siagi
  •  vijio vya mezani viwili vya sosi ya matofaa
  •  mayai mawili
  •  kijiko cha chai kimoja cha vanilla
  •  kikombe kimoja nusu cha maziwa


Maelekezo:
1.     Choma kiazi kitamu. Washia moto tanuri kwa digrii 425. Osha kiazi kitamu na toboa mara nyingi. Weka foilo katika karatasi ya kuoka na weka kiazi kitamu katika karatasi ya kuoka. Choma kwa saa moja. Acha kiwe baridi.
2.     Washia moto tanuri kwa digrii 350.
3.     Katika bakuli, kuroga unga, chumvi, soda ya kuoka, hamira, mdalasini, na kungumanga.
4.     Katika bakuli nyingine, piga ndani ya kiazi kitamu, sukari, sukari ya kahawia. Ongeza siagi, sosi ya matofaa na mayai. Piga vanilla.
5.     Ongeza nusu ya unga mchanganyiko katika kiazi kitamu mchanganyiko na piga. Ongeza nusu ya maziwa na piga. Rudia.  Mwaga gonga katika sufuria ya mkate na kuoka kwa saa moja.

Maagizo ya Upishi wa Kuki ya Sukari

Siku ya Krismasi, familia wangu sisi hupika kuki ya sukari. Nina makumbuko mengi ya familia yangu na mimi tunaunda unga uliokandwa, tunaunyooka, tunaukata, tunauoka, na tunaupamba. Ninapenda kuki sana kwa sababu inakuwa tamu na inapokuwa pamba, ina rangi nyingi. Pia, maagizo ya upishi haya yanaunda kuki nyini sana sana sana!!


Viungo:
Kuki:
  •        kikombe kimoja na nusu cha siagi
  •        vikombe viwili vya sukari
  •        mayai manne
  •        kijiko cha mezani cha vanilla
  •        vikombe vitano vya unga
  •        vijiko vya mezani vya soda ya kuoka
  •        kijiko cha mezani cha chumvi


“Frosting”
  •        vikombe vinne vya sukari ya ungaunga
  •        kikombe nusu cha siagi
  •        vijiko vya chai viwili vya maziwa
  •        kijiko cha mezani cha vanilla
  •        rangi ya kuongeza katika chakula


Maelekezo:

1. Katika bakuli kubwa, piga siagi na sukari. Ongeza mayai na vanilla na piga.

2. Ongeza unga, soda ya kuoka na chumvi na piga. Funika na poa katika “refrigerator” kwa saa moja.

3. Washa moto tanuri hadi digrii mia nne. Nyoosha unga uliokandwa katika bodi yenye kuwa visha kidogo kwa unga. Nyoosha unga uliokandwa katika inchi robo. Kata unga uliokanda kwa kutumia kikata kuki. Hamisha katika sufuria ya kuoka na kuoka kwa dakika sita kwa kumi. Poesha kabisa mbele pamba kwa “frosting.”


4. Katika bakuli, piga siagi na sukari ya ungaunga. Ongeza maziwa na vanilla na piga kwa dakika nyingi hata inakuwa ngumu. Ongeza food coloring na pamba kuki!

Maagizo ya Upishi wa Mkate wa Ndizi

Ninapenda kupika mkate. Ninapenda mkate wa ndizi, mkate wa viazi vitamu, mkate wa karoti, mkate wa mboga na mkate wa “zucchini.” Haya maagizo ya upishi ni ya nyanya yangu. Nilipokuwa mdogo na alikuja nyumba yangu, alileta kila wakati mkate huu. Sasa, ninaipikia timu ya gofu yangu mkate tunapoenda mashindano. Ninafikiri tunashinda kwa sababuya mkate :) 


Viungo:
  •       kikombe nusu cha siagi
  •        kikombe kimoja cha sukari
  •        mayai mawili
  •        kijiko cha mezani nusu cha chumvi
  •        kijiko cha mezani cha vanila
  •        kijiko cha mezani cha soda ya kuoka
  •        vikombe viwili vya unga
  •        ndizi tatu mbivu, yenye kuseta


Maelekezo:

1. Washa tanuri moto hadi digrii mia tatu. Ongeza mafuta kidogo na unga dogo katika sufuria ya mkate ili haiambati.

2. Katika bakuli, piga siagi na sukari. Ongeza mayai, chumvi, na vanilla na kuroga. Ongeza soda ya kuoka na unga na piga. Ongeza ndizi yenye kuseta na koroga. Mwaga katika sufuria ya mkate na uoke kwa saa moja.


Thursday, December 5, 2013

Maagizo ya upishi Mandazi


Siku ya alhamisi iliyopita, nilipika chakula cha jio kutoka chama cha Half the Sky. Kiini cha chajio kilikuwa Afrika ya mashariki. Nilipika viazi, mchuzi wa choroko, wali na mandazi. Mandazi yalikuwa sahani bora na watu wote waliipenda!


Viungo:
  •        yai moja
  •        kikombe nusu cha sukari
  •        kikombe cha nusu cha maziwa
  •        vijiko vya mezani viwili vya siagi, yenye kuyeyuka
  •        vikombe viwili vya unga
  •        vijiko vya chai viwili vya hamira
  •        Mafuta


Maelekezo:

1. Katika bakuli, ongeza viungo vyote na koroga. Weka sufuria katika jiko na washa moto. Weka mafuta katika mtungi ili kwamba inakuwa inchi mbili za mafuta. 

2. Nyooka unga uliokandwa katika bodi yenye kuwa visha kidogo kwa unga. Nyooka unga uliokandwa katika inchi ya nne moja. Kata unga uliokandwa katika pembe tatu na weka katika mafuta moto. 

3. Kaanga hata mandazi yanakuwa ya rangi ya kahawia katika pande zote. Taratibu ondoa mandazi ya mafuta na kausha kwa taulo.

Maagizo ya upishi kuchoma makorosho ya rosemary

Nilipika makorosho haya kutoka likizo ya Thanksgiving mwaka uliopita. Yalikuwa mazuri sana na watu wote waliyakula haraka pia! Halafu, nilipika hayo kutoka chama na marafiki na tena, watu wote waliyakula haraka sana! Mungu wangu, nilijifikiri.  Watu waliyapenda! Sasa, ninayapika muda wote kwa sababu ni rahisi kupika na ninayapenda na marafiki wanayapenda pia!


Viungo:
  •        kilo nusu ya makorosho
  •        vijiko vya mezani viwili vya majani ya rosemary, katakata
  •        kijiko cha chai nusu cha unga cha cayenne
  •        vijiko vya chai viwili vya sukari ya kahawia
  •        vijiko vya chai viwili vya chumvi
  •        kijiko cha mezani kimoja cha siagi yenye kuyeyuka


Maelekezo:

1. Washa tanuri moto hadi digrii 375.

2. Weka makorosho katika sufuria ya kuoka na uoke kwa dakika saba au nane. Angalia makorosho kuyakini hayapikiki haraka pia.

3. Katika bakuli nyingine, ongeza rosemary, pilipili iliyosagwa aina ya cayenne, sukari ya kahawia, chumvi na siagi na koroga.

4. Makorosho yanapoisha kupika, yaruhusu kupoa kutoka dakika mbili au tatu. Mwaga makorosho katika bakuli na koroga hata makorosho yote kuvisha.




Keki ya boga na mtama

Katika msimu wa vuli, watu wengi wanapika kwa boga kwa sababu huu ni msimu wa kuvuna boga. Watu wanaweka boga katika kila chakula: pankeki, saladi, na nyama, na wali, na katika keki. Hiki chakula ni keki ya boga na mtama. Millet ni punje kama wali walakini ni ngumu kidogo. Keki ni nyevu na mtama ongeza ladha mpya. Keki ni nzuri sana, sana sana.


Viungo:
  •        kikombe nusu cha punje ya mtama
  •        yai moja
  •        kikombe nusu cha krimi aina ya ‘sour cream’
  •        kikombe nusu cha maziwa
  •        vijiko vya mezani vinne vya siagi, iliyoyeyuka
  •        kikombe kimoja cha boga chenye kuseta
  •        kikombe theluthi moja cha sukari
  •        kikombe theluthi moja cha sukari ya kahawia
  •        vikombe viwili vya unga
  •        kijiko cha chai kimoja cha hamira
  •        kijiko cha chai nusu cha soda ya kuoka
  •        kijiko cha chai nusu cha chumvi
  •        kijiko cha chai nusu cha mdalasini
  •        kijiko cha chai robo cha kungumanga
  •        kijiko cha chai robo cha karafuu yenye kusaga


Maelekezo:

1. Washa moto tanuri hadi digrii mia nne. Weka gazeti ainya ya ‘muffin’ katika sufuria ya keki.

2. Washa jiko moto wastani. Weka mtungi katika jiko na ongeza mtama. Choma millet kwa dakika tatu au nne, hata inafanya sauti ya “pop.”

3. Katika bakuli, kuroga yai, sour cream, maziwa, siagi, boga, sukari, na sukari ya kahawia. Katika bakuli nyingine, ongeza unga, hamira, soda ya kuoka, chumvi, mdalasini, kungumanga, na karafuu yenye kusaga. Ongeza unga mchanganyiko katika boga mchanganyiko na koroga.


4. Teka mchanganyiko katika vikombe vya keki. Jaa vikombe vya keki. Oka kwa dakika ishirini na tano. Ruhusu keki kuzimua kwa dakika tano.