Nilipika makorosho haya kutoka likizo ya Thanksgiving mwaka uliopita.
Yalikuwa mazuri sana na watu wote waliyakula haraka pia! Halafu, nilipika hayo
kutoka chama na marafiki na tena, watu wote waliyakula haraka sana! Mungu
wangu, nilijifikiri. Watu
waliyapenda! Sasa, ninayapika muda wote kwa sababu ni rahisi kupika na
ninayapenda na marafiki wanayapenda pia!
Viungo:
- kilo nusu ya makorosho
- vijiko vya mezani viwili vya majani ya rosemary, katakata
- kijiko cha chai nusu cha unga cha cayenne
- vijiko vya chai viwili vya sukari ya kahawia
- vijiko vya chai viwili vya chumvi
- kijiko cha mezani kimoja cha siagi yenye kuyeyuka
Maelekezo:
1. Washa tanuri moto hadi digrii 375.
2. Weka makorosho katika sufuria ya kuoka na uoke kwa dakika
saba au nane. Angalia makorosho kuyakini hayapikiki haraka pia.
3. Katika bakuli nyingine, ongeza rosemary, pilipili
iliyosagwa aina ya cayenne, sukari ya kahawia, chumvi na siagi na koroga.
4. Makorosho yanapoisha kupika, yaruhusu kupoa kutoka dakika
mbili au tatu. Mwaga makorosho katika bakuli na koroga hata makorosho yote
kuvisha.
No comments:
Post a Comment