Karibu!

Karibu rafiki! Ninaitwa Mackenzie. Mimi ni mwanafunzi Washington University mjini St. Louis katika jimbo la Missouri. Ninafanya blogu hii kama maradi wa mwisho wa darasa langu la kiswahili. Ninatumaini unapenda maagizo ya upishi yangu! Asante sana kwa kusoma blogu yangu. Nina blogu ya kupika nyingine katika kiingereza, uangalie: http://neverskipdessertbymackenzie.wordpress.com

Tuesday, December 10, 2013

Maagizo ya Upishi wa Mkate wa Viazi Vitamu

Mwaka uliopita, nilipika viazi vitamu kila wakati. Nilivipika katika kila kitu! Siku moja, nilifikira kuweka viazi vitamu katika mkate. Nilipenda ndizi katika mkate wa ndizi kwa hivyo, pengine viazi vitamu katika mkate vitakuwa vizuri pia! Niliupopika mkate ulikuwa mzuri sana na mimi na rafiki yangu tuliupenda! Sasa, ninapika mkate huu kila wakati. Pia, mwaka uliopita niliupika kutoka darasa la kiswahli na wanafunzi waliupenda! 


Viungo:
  •  kikombe kimoja na nusu cha unga
  •  kijiko cha chai kimoja cha chumvi
  •  kijiko cha chai kimoja cha soda ya kuoka
  •  kijiko cha chai kimoja nusu cha hamira
  •  kijiko cha chai kimoja nusu cha mdalasini
  •  kijiko cha chai kimoja nusu cha kungumanga
  •  ndani ya kiazi kitamu kimoja
  •  kikombe thelathi mbili cha sukari
  •  kikombe theluthi moja cha sukari ya kahawia
  •  vijiko vya mezani sita vya siagi
  •  vijio vya mezani viwili vya sosi ya matofaa
  •  mayai mawili
  •  kijiko cha chai kimoja cha vanilla
  •  kikombe kimoja nusu cha maziwa


Maelekezo:
1.     Choma kiazi kitamu. Washia moto tanuri kwa digrii 425. Osha kiazi kitamu na toboa mara nyingi. Weka foilo katika karatasi ya kuoka na weka kiazi kitamu katika karatasi ya kuoka. Choma kwa saa moja. Acha kiwe baridi.
2.     Washia moto tanuri kwa digrii 350.
3.     Katika bakuli, kuroga unga, chumvi, soda ya kuoka, hamira, mdalasini, na kungumanga.
4.     Katika bakuli nyingine, piga ndani ya kiazi kitamu, sukari, sukari ya kahawia. Ongeza siagi, sosi ya matofaa na mayai. Piga vanilla.
5.     Ongeza nusu ya unga mchanganyiko katika kiazi kitamu mchanganyiko na piga. Ongeza nusu ya maziwa na piga. Rudia.  Mwaga gonga katika sufuria ya mkate na kuoka kwa saa moja.

No comments:

Post a Comment