Ninapenda kupika mkate. Ninapenda mkate wa ndizi, mkate wa
viazi vitamu, mkate wa karoti, mkate wa mboga na mkate wa “zucchini.” Haya
maagizo ya upishi ni ya nyanya yangu. Nilipokuwa mdogo na alikuja nyumba yangu,
alileta kila wakati mkate huu. Sasa, ninaipikia timu ya gofu yangu mkate tunapoenda
mashindano. Ninafikiri tunashinda kwa sababuya mkate :)
Viungo:
- kikombe nusu cha siagi
- kikombe kimoja cha sukari
- mayai mawili
- kijiko cha mezani nusu cha chumvi
- kijiko cha mezani cha vanila
- kijiko cha mezani cha soda ya kuoka
- vikombe viwili vya unga
- ndizi tatu mbivu, yenye kuseta
Maelekezo:
1. Washa tanuri moto hadi digrii mia tatu. Ongeza mafuta kidogo
na unga dogo katika sufuria ya mkate ili haiambati.
2. Katika bakuli, piga siagi na sukari. Ongeza mayai,
chumvi, na vanilla na kuroga. Ongeza soda ya kuoka na unga na piga. Ongeza
ndizi yenye kuseta na koroga. Mwaga katika sufuria ya mkate na uoke kwa saa
moja.
No comments:
Post a Comment